1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za Umoja wa ulaya zimejitolea kuipatia Marekani mafuta ya petroli.

3 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEeo

Nchi za Umoja wa Ulaya zimeamua kuipatia Marekani mafuta ya petroli ili kusaidia kupunguza uhaba wa mafuta uliosababishwa na kimbunga Katrina nchini humo.Ujerumani pia itajiunga na mpango huo unaosimamiwa na shirika la kimataifa la nishati.Katika kipindi cha siku 30 zijazo,mapipa milioni 60 ya mafuta yatawasilishwa sokoni-shirika hilo la kimataifa limesema.Karibu nusu ya shehena hiyo inatokea katika nchi za Umoja wa Ulaya.Wakati huo huo visima vya mafuta katika eneo la kusini la Marekani vimeanza kidogo kidogo kufanya kazi.