1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michelle Bachelet atoa wito wa kuangamizwa utumwa na ubaguzi

Zainab Aziz Mhariri:Yusuf Saumu
12 Julai 2021

Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amezitaka nchi za ulimwengu zichukue hatua kabambe za kushughulikia maovu ya utumwa, ukoloni na ubaguzi wa rangi ikiwa pamoja na kulipa fidia.

https://p.dw.com/p/3wNcM
Hochkommissarin für Menschenrechte Michelle Bachelet
Picha: Martial Trezzini/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Mkuu huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amewasilisha ripoti juu ya mfumo wa ubaguzi wa rangi na kukiukwa haki za binadamu za waafrika na watu wenye asili ya Afrika.

Katika ripoti yake Bachelet hususan alirelejea kifo cha mmarekani mweusi George Floyd na mauaji ya watu weusi kwa ujumla nchini Marekani. Ripoti ya bibi Bachelet iliyowailishwa kwenye kikao cha 47 cha Baraza la Haki za Binadamu mwaka mmoja tangu kuuliwa kwa George Floyd ina shabaha ya kujenga mwendelezo wa kuiamrisha uchunguzi wa masahibu ya ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi duniani kote.

Picha ya marehemu George Floyd aliyeuawa na polisi wa Marekani
Picha ya marehemu George Floyd aliyeuawa na polisi wa MarekaniPicha: DW

Michelle Bachelet ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwamba utafiti uliofanywa haukubainisha mfano wa hata nchi moja iliyochunguza kwa ukamilifu, iliyoyafanya mnamo miaka iliyopita na jinsi maisha ya watu weusi yalivyoathirika licha ya juhudi za kutafuta ukweli na kuchukua hatua za kisheria. Bachelet amesema watu weusi wanabaguliwa kwa namna mbalimbali:

Mkuu huyo wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa amesema katika ripoti yake kwamba mara nyingi watu wenye asili ya Afrika wanaishi maisha ya kimasikini, wanalipwa mishahara ya chini na wanafanya kazi ambazo hazina ustadi. 

Amesema watu hao wanabaguliwa pia wanapotafuta nyumba na amezitaka nchi zote zichukue hatua ili kuanzisha na kugharamia kikamilifu michakato ya kubainisha ukweli kwa kuwashirikisha waathiriwa katika jamii zao.

Waandamanji mjini London, Uingereza wanaopinga ubaguzi wa rangi
Waandamanji mjini London, Uingereza wanaopinga ubaguzi wa rangiPicha: Wiktor Szymanowicz/NurPhoto/picture alliance

Kamishna wa haki za binadamu Michelle Bachelet amesema inapasa kuyajua madhara yaliyowafika watu weusi na athari zinazoedelea kuwasibu. Kaimu balozi wa Marekani mjini Geneva Benjamin Moeling ameiunga mkono ripoti ya Umoja wa Mataifa katika tamko alilotoa kwa njia ya video. Amesema Marekani inayashughulikia maswala hayo ndani na nje kwa dhati na kwa njia ya uwazi. Amesema Marekani inaikabili mizizi ya ubaguzi wa rangi na matumizi ya nguvu kupita kiasi yanayofanywa na polisi.

Vyanzo:/AP/AFP