1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Suluhisho la mataifa mawili lapigiwa debe huko Barcelona

28 Novemba 2023

Mataifa ya kiarabu na Umoja wa Ulaya yamekubaliana kuwa kuundwa mataifa mawili ndiyo suluhu ya uhakika kwa mzozo kati ya Israel na Palestina.

https://p.dw.com/p/4ZVYJ
Israel I Jerusalem Magharibi
Mji wa Jerusalem ni moja ya maeneo tete katika kufikia lengo la pendekezo la kuundwa mataifa mawili yaani, Palestina na Israel.Picha: Chris McGrath/Getty Images

Mtazamo huo umeelezwa wakati wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka mataifa ya Ulaya na ya kiarabu uliofanyika jana mjini Barcelona nchini Uhispania.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borell, amesema mataifa yote wanachama wa umoja huo pamoja na wawakilishi wa mataifa mengine karibu yote yaliyohudhuria mkutano wa Barcelona, yameafikiana juu ya umuhimu wa suluhisho la kuundwa madola mawili.

Mwanadiplomasia huyo pia amependekeza Mamlaka ya Palestina inayotawala sana eneo la Ukingo wa Magharibi ndiyo iwe na jukumu la utawala pia kwenye Ukanda wa Gaza.

Pendekezo la suluhisho la mataifa mawili linajumuisha kuundwa kwa taifa la Palestina kwenye ardhi ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza likiwa jirani na Israel.