1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi tajiri za G7 zatuma ujumbe mzito kwa China na Urusi

22 Mei 2023

Viongozi wa nchi tajiri kiviwanda duniani za kundi la G7 wametuma ujumbe mzito kwa Urusi na China kufuatia mkutano wao wa kilele wa siku tatu uliofanyika nchini Japan, ambao pia ulitowa msimamo wa kuisadia zaidi Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Ret0
G7 Summit in Hiroshima
Picha: Susan Walsh/REUTERS

Viongozi hao wametangaza kuchukua msimamo mkali kuelekea azma ya China ya kutaka kutanuwa ushawishi wake duniani, licha ya nchi hizo kuitegemea Beijing kiuchumi.

Rais Volodymyr Zelensky ambaye pia alihudhuria mkutano huo, aliwahutubia viongozi wa G7  jana jumapili. Kadhalika rais huyo wa Ukraine alifanya mazungumzo na rais wa Marekani Joe Biden aliyeahidi kumpatia msaada zaidi wa kijeshi wa thamani ya dola milioni 375.

Soma pia:G7: Ukraine yatawala siku ya mwisho ya mkutano wa kilele 

Msaada huo utajumuisha bunduki, makombora pamoja na magari ya kijeshi Ukraine. Aidha  Washington pia imetoa idhini ya kupelekwa ndege za kivita aina ya F-16 nchini Ukraine kama sehemu ya mpango wa pamoja wa washirika, ukiungwa mkono na Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Denmark na Ureno. Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz nae ametilia mkazo uungaji mkono wa kundi hilo la G7 kwa Ukraine.