1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Nawaz Sharif kushiriki uchaguzi wa bunge Pakistan

27 Desemba 2023

Chama cha Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif, kimesema kiongozi wake atawania kipindi cha nne madarakani, kikisisitiza kuwa Sharif atakuwa mgombea wake katika uchaguzi ujao wa bunge na ofisi ya Waziri Mkuu.

https://p.dw.com/p/4acAr
Pakistan Lahore | Waziri Mkuu wa zamani Pakistans Nawaz Sharif
Waziri Mkuu wa zamani Pakistans Nawaz Sharif ambae atawania kipindi cha nne madarakani.Picha: Ali Kaifee/DW

Sharifaliyewahi kuwa Waziri Mkuu mara tatu, alirejea Pakistan mwezi Oktoba mwaka huu baada ya kukaa uhamishoni mjini London kwa miaka minne, kuepuka kutumikia kifungo chake kwa makosa ya ufisadi. 

Soma pia:Kwanini Wapakistan hawajali kuhusu uchaguzi ujao

Hata hivyo hukumu na kifungo dhidi yake vilibatilishwa baada ya kukatiwarufaa aliporejea nyumbani, hatua iliyomfungulia njia kuwania nafasi bungeni. Bunge hilo litamteua Waziri Mkuu mpya baada ya uchaguzi huo wa tarehe 8 Februari.