1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yajadili kuongeza kiwango cha matumizi ya ulinzi

15 Februari 2023

Wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wameanzisha mjadala leo kuhusu suala tete la kuongeza kiwango cha kitaifa cha gharama ya ulinzi baada ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine kuathiri usalama wao.

https://p.dw.com/p/4NWC9
Brüssel Treffen NATO-Verteidigungsminister | Boris Pistorius
Picha: JOHANNA GERON/REUTERS

Uvamizi wa Moscow dhidi ya Kyiv umeshuhudia msururu wa washirika wa Ulaya wakidhamiria kutumia mabilioni zaidi ya euro kwenye vikosi vyao vya jeshi. 

Baadhi katika muungano huo wa kijeshi sasa wanashinikiza kujumuishwa nyongeza hizo kwa kutumia mkutano wa kilele ujao mjini Vilnius mwezi Julai kupandisha kiwango cha sasa cha NATO cha asilimia mbili ya pato jumla la ndani. 

Washirika wa Ukraine wajadili namna ya kuipa silaha zaidi

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius ameuambia mkutano wa mawaziri wenzake wa NATO mjini Brussels leo kuwa anaamini kutaka tu kuliangalia suala hilo kwa kuunga mkono kiwango cha asilimia mbili haitoshi. Lakini baadhi ya mataifa yanasitasita kukiwanya kiwango hicho kuwa kikubwa zaidi.