1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yaanza luteka za kijeshi pamoja na wanachama wake wapya

4 Machi 2024

Vikosi vya jumuiya ya kijeshi ya NATO leo vinaanza luteka za kijeshi juu ya kulilinda eneo lake jipya la ulaya kaskazini.

https://p.dw.com/p/4d8Hx
Ndege ya Kivita chapa F-16
Ndege aina ya F-16 ikiwa anganiPicha: Mindaugas Kulbis/AP Photo/picture alliance

Zaidi ya wanajeshi 20,000 kutoka mataifa 13 watashiriki katika mazoezi hayo yatakayochukua karibu wiki mbili kwenye mikoa ya kaskazini ya Finland, Norway na Sweden.

Wanajeshi zaidi ya 4,000 wa Finland, ambayo ni mwanachama mpya wa NATO, wanashiriki kwa mara ya kwanza katika operesheni ya ulinzi wa pamoja wa kikanda kwenye muungano huo.