1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

NATO kuongeza kikosi cha kulinda amani Kosovo

30 Septemba 2023

Jumuiya ya kujihami ya NATO imesema iko tayari kuongeza kikosi cha kulinda amani Kosovo kufuatia mapigano makali yaliyozuka hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4WzVe
Rais wa Kosovo Vjosa Osmani (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
Rais wa Kosovo Vjosa Osmani (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa NATO Jens StoltenbergPicha: Office of the Kosovo Presidency

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameeleza kuwa "ameidhinisha vikosi vya ziada ili kushughulikia hali ya sasa."

Taarifa yake hata hivyo haikutoa maelezo zaidi, japo wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema imetenga kikosi cha wanajeshi kati ya 500 na 650 iwapo watahitajika katika oparesheni ya kulinda amani. Kikosi hicho kinajulikana kama KFOR.

Kikosi hicho kiliwasili Kosovo hivi karibuni kwa ajili ya kufanya luteka za kijeshi za muda mrefu.