1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Kosovo yaitaka Serbia kuwakabidhi washukiwa wa mashambulizi

25 Septemba 2023

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kosovo Xhelal Svecla amesema washukiwa sita wa ufyatuaji risasi eneo la mpakani walivuka na kuingia Serbia.

https://p.dw.com/p/4Wmku
Xhelal Svecla, waziri wa mambo ya Ndani ya Kosovo.
Xhelal Svecla, waziri wa mambo ya Ndani ya Kosovo.Picha: Olivier Matthys/AP/dpa/picture alliance

Waziri huyo ametoa wito, watu hao wakabidhiwe kwa mamlaka husika nchini humo.

Waziri huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa Kulingana na taarifa walizo nazo hadi sasa, magaidi sita waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Novi Pazar kusini mwa Serbia, na wanaiomba Belgrade kuwakabidhi mara moja kwa mamlaka ya Kosovo, ili waweze kukabiliwa na mkono wa sheria.

Marekani imelaani makabiliano hayo ya umwagaji damu kati ya wanajeshi wa Kosovo na watu wenye silaha karibu na mpaka wa Serbia. Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amezitolea wito Kosovo na Serbia kujiepusha na vitendo au kauli zinazoweza kuchochea zaidi hali hiyo.

Kosovo ilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Serbia mwaka 2008 ingawa utawala wa Belgrade pamoja na washirika wake, China na Urusi bado hazitambui hatua hiyo ya Kosovo.