1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI: Somalia yaomba msaada kupambana na wanamgambo wanaoziteka nyara meli za umoja wa mataifa

22 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEPN

Serikali ya Somalia inataka isaidiwe na jamii ya kimataifa kupamba na makundi ya wanamgambo wa kisomali ambao wameongeza mashambulio dhidi ya meli zilizokodishwa na umoja wa mataifa.

Mwito huo umetolewa siku moja baada ya ripoti kuchapishwa inayosema mashambulio yamezidi katika pwani ya kusini na mashariki mwa Somalia, eneo muhimu linaloiunganisha bahari nyekundu na bahari ya Hindi.

Somalia haijakuwa na serikali yenye mamlaka tangu upinzani ulipomuondoa madarakani dikteta Mohamed Siad Barre mwaka wa 1991.