1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neuer bado sana kurejea kikosini Bayern Munich

7 Agosti 2023

Wakati ligi ya Bundesliga ikikaribia kuanza, nahodha wa Bayern Munich Manuel Neuer amefanyiwa upasuaji wa kuondoa vyuma ambavyo vitamuweka nje ya uwanja kwa muda usiojulikana.

https://p.dw.com/p/4Us9h
Fußball | Manuel Neuer
Manuel Neuer, Kipa na nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani.Picha: Soeren Stache/dpa/picture alliance

Mlinda lango wa Bayern Munich Manuel Neuer amefanyiwa upasuaji mdogo wa kuondoa vipandikizi vya chuma kwenye mguu wake uliovunjika msimu uliopita.

Bayern wamesema leo kuwa "Nahodha wa FC Bayern ameanza tena mazoezi mepesi mara moja ya kujiimarisha." 

Kuna uwezekano mdogo kwa mlinda lango huyo kurejea kikosini katika michezo ya Bayern ya hivi karibuni na haijawekwa wazi ni lini tena atarejea kuanza mazoezi kamili kuelekea kujiunga na kikosi cha Bayern Munich. 

Soma zaidi: Kane kujiunga na Bayern? Füllkrug kuhamia Leverkusen?

Mchezo wa kwanza wa Bayern msimu huu ni Jumamosi ya Agosti 12 dhidi ya Leipzig katika Kombe la Super Cup la Ujerumani kabla ya kutetea ubingwa wake wa Bundesliga kuanzia mnamo Agosti 18 huko Werder Bremen.

Manuel Neuer mwenye umri wa miaka 37 hajacheza tangu michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana baada ya kuvunjika mguu katika ajali ya kuteleza kwenye theluji mwezi Disemba. Hakuwa kwenye ziara ya kabla ya msimu mpya ya Bayern nchini Japan na Singapore.

Fussball Weltmeisterschaft | Vorrundenspiel Costa Rica - Deutschland
Manuel Neuer amefanyiwa tena operesheni ya kuondoa vyuma na hali hiyo itamfanya kuchelewa kureeja dimbani.Picha: Laci Perenyi/IMAGO

Bayern Munich ilimsajili kipa wa Uswizi Yann Sommer kama mrithi wa Manuel Nuer na kipa huyo sasa anatajwa kuwindwa na makamu bingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Inter Milan.

Klabu hiyo ya Ujerumani pia inammezea mate mshambuliaji na nahodha wa England Harry Kane ambapo inaelezwa kuwa Tottenham Hotspurs imegoma kuchukua kiasi cha Euro Milioni 100 kilichotolewa na Bayern Munich kuinasa saini ya nyota huyo.