1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kane kujiunga na Bayern? Füllkrug kuhamia Leverkusen?

12 Julai 2023

Bayern Munich bila shaka wanataka kumsaini nahodha wa England Harry Kane na wanaweza hata kusubiri hadi mwaka ujao kama hawatompata staa huyo wa Tottenham Hotspur katika dirisha hili la usajili

https://p.dw.com/p/4Tm3x
Fußball-WM Katar 2022 | England v Iran
Picha: Javier Garcia/Shutterstock/IMAGO

Bayern Munich bila shaka wanataka kumsaini nahodha wa England Harry Kane na wanaweza hata kusubiri hadi mwaka ujao kama hawatompata staa huyo wa Tottenham Hotspur katika dirisha hili la usajili.

Jarida la michezo la kila wiki Ujerumani la Sport Bild limesema Kane mwenye umri wa miaka 29 ameashiria kuwa angeweza pia kusubiri kwa miezi mingine 12 ili kujiunga na mabingwa hao mara 11 wa Bundesliga ambao kisha itakuwa ni uhamisho huru.

Mshambuliaji huyo wa England Kane na Bayern inaripotiwa wamefikia makubaliano lakini ofa za euro milioni 70 na milioni 80 hazijazingatiwa kuwa nzuri vya kutosha na mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy anayesemakana kuhitaji karibu euro pauni 100

Leverkusen yamuwinda Füllkrug

Fussball 1. Bundesliga 1.FSV Mainz 05 - SV Werder Bremen | Niclas Füllkrug
Leverkusen wanamuwinda Füllkrug kutoka BremenPicha: Bratic/nordphoto GmbH/picture alliance

Bayer Leverkusen wanaripotiwa kuhitaji huduma za  mshambuliaji wa Ujerumani Niclas Füllkrug kutoka mahasimu wao wa Bundesliga Werder Bremen kwa sababu Patrick Schick ataendelea kuwa mkekani hadi Oktoba.

Bayer tayari wamemsaini mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Jonas Hofmann na kiungo wa Kiswisi Granit Xhaka, na jarida la Bild limeropoti kuwa Füllkrug sasa yuko kwenye rada yao.

Neuer kurejea

Ripoti na vipimo vya matibabu vya Manuel Neuer vimekuwa vizuri huku kipa huyo wa Ujerumani na Bayern Munich akirejea mazoezini baada ya kupona jeraha la mguu alilopata Desemba mwaka jana.

Neuer mwenye umri wa miaka 37, anafanya mazoezi chini ya mwalimu wa makipa, na daktari wa viungo, ijapokuwa haijafahamika wazi kama atakuwa sehemu ya kambi ya mazoezi ya kabla ya kuanza msimu mpya.

Inasubiriwa kuona kama Neuer atarejea katika ubora wake wa zamani lakini naibu yake halisi, Alexander Nübel, inaripotiwa kuwa anaondoka klabuni hapo.