1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Somalia: Tutawatimua wanajeshi wa Ethiopia

3 Juni 2024

Somalia imesema itawafukuza maelfu ya wanajeshi wa Ethiopia waliopo nchini humo kulinda amani iwapo Ethiopia haitoyafuta makubaliano yanayozozaniwa ya bandari na jimbo lililojitenga la Somaliland.

https://p.dw.com/p/4gb0c
Somaliland| Berbera 2024 | Ethiopia
Bandari ya Berbera huko Somaliland imekuwa chanzo cha mzozo kati ya Somalia na Ethiopia.Picha: Eshete Bekele/DW

Taarifa hii ni kulingana na afisa mwandamizi wa Somalia mapema leo.

Mshauri wa usalama wa taifa Hussein Sheikh-Ali ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanajeshi wote wa Ethiopia na waliopelekwa chini ya makubaliano ya nchini mbili watalazimika kuondoka, ikiwa taifa hilo haliutafuta mkataba huo kabla ya mwishoni mwa Juni.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia na jeshi, ENDF hakupatikana kuzungumzia hilo.

Karibu wanajeshi 3,000 wamekita kambi katika taifa hilo la Pembe ya Afrika kama sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika, ATMIS wanaopambana na kundi la al-Shabaab, linalodhibiti eneo kubwa la Somalia.