1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Somalia afuta mkataba wa Somaliland na Ethiopia

Josephat Charo
7 Januari 2024

Rais wa Somalia ameufuta mkataba kati ya Somaliland na Ethiopia ulioiwezesha Ethiopia kuitumia bahari ya Shamu.

https://p.dw.com/p/4ax75
Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh MohamudPicha: Feisal Omar/REUTERS

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesaini sheria kubatilisha mkataba wa jimbo lililojitenga la Somaliland unaoipa Ethiopia uwezo wa kuifikia Bahari ya Shamu kwa mabadilishano wa kutambuliwa jimbo hilo kama taifa huru.

Azma ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuweza kuitumia bahari hiyo imezua msuguano kati ya Ethiopia na majirani zake na kuibua wasiwasi wa kuzuka machafuko mapya katika eneo hilo. Somalia ambayo inaiona Somaliland kama himaya yake, iliyakataa makubaliano hayo yaliyotiwa saini siku ya mwaka mpya.