1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaituhumu Urusi kwa vitendo vya mateso dhidi ya raia

11 Septemba 2023

Mwangalizi wa Umoja wa Mataifa ameishutumu Urusi kwa kutumia makusudi vitendo vya mateso kama sera ya serikali ya Moscow katika vita vyake dhidi ya Ukraine, kwa lengo la kuzusha hali ya hofu miongoni mwa raia.

https://p.dw.com/p/4WB4s
Ukraine-Krieg Kiew Schewtschenko | Kriegsschäden
Picha: John Moore/Getty Images

Alice Jill Edwards amesema kumekuwepo na madai ya kuaminika ya mateso na matendo mengine yanayokiuka haki za binaadamu yanayoendeshwa na mamlaka za urusi dhidi ya raia na mateka wa vita.

Mwangalizi huyo wa  Umoja wa Mataifa  alifanya ziara ya wiki moja nchini Ukraine na kuzungumza na mashuhuda waliomueleza kuwa wanajeshi wa Urusi huwatesa watu kwa kutumia shoti za umeme hadi kwenye sehemu zao za siri, kuwapiga, kuwatishia kunyongwa, kubakwa au kuuawa.

Kulingana na serikali ya Ukraine, zaidi ya visa 103,000 vya uhalifu wa kivita vimeorodheshwa.