1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkereketwa wa Putin ajeruhiwa baada ya gari lake kulipuka

6 Mei 2023

Mwandishi riwaya Zakhar Prilepi, anayeunga mkono utawala wa rais Vladimir Putin, amejeruhiwa baada ya gari lake kulipuka. Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la serikali ya Urusi,TASS.

https://p.dw.com/p/4Qzbz
Russland Vladimir Putin per Video nimmt an der Einweihung des türkischen Kernkraftwerks Akkuyu teil
Picha: SPUTNIK via REUTERS

Mwandishi riwaya Zakhar Prilepi, anayeunga mkono utawala wa rais Vladimir Putin, amejeruhiwa baada ya gari lake kulipuka. Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la serikali ya Urusi,Tass, Dereva wake amekufa kutokana na mlipuko huo. Mkasa huo ulitokea kwenye jimbo la Nizhny Novgorod, umbali wa kilometa 400 mashariki ya mji mkuu wa Urusi, Moscow. Hii ni mara ya tatu kutokea mkasa kama huo kwa watu wanaounga mkono utawala wa Putin tangu kuanza kwa vita vya nchini Ukraine. Mnamo mwezi wa Agosti mwaka uliopita, binti yake mtaalamu wa nadharia za kisiasa, Daria Dugina pia alikufa kutokana na mlipuko ndani ya gari katika kitongoji kimoja cha mji wa Moscow. Baba yake alizingatiwa kuwa mshauri wa rais Putin. Polisi nchini Urusi wameanzisha uchunguzi. Wakati huo huo wizara ya mambo ya ndani ya Urusi imesema mtu anayetuhumiwa kuhusika na shambulio hilo amekamatwa.