1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wairan kufanya uchaguzi wa marudio Julai 5

29 Juni 2024

Mamlaka ya uchaguzi ya Iran imetangaza kuwa mgombea wa mrengo wa mabadiliko Masoud Pezeshkian na mhafidhina Saeed Jalili watakwenda katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4hf0s
Kabla ya uchaguzi wa Iran | Mgombea Massoud Peseschkian
Tehran, Iran, Mgombea mageuzi katika uchaguzi wa rais wa Irani Massoud mnamo Juni 28, 2024. Picha: Vahid Salemi/dpa/AP/picture alliance

Pezeshkian alipata karibu asilimia 42.5 ya kura na Jalili akafuata kwa asilimia 38.7. Lakini pia kuna wagombea wengine wawili katika kinyang'anyiro hicho.

Kwa kuwa hakuna aliyepata idadi kubwa kabisa ya kumfanya aunde serikali, tumeimetangaza kuwa duru ya pili ya uchaguzi ifanyike Julai 5.

Takriban wapiga kura milioni 61 nchini Iran hapo Ijumaa walikuwa na haki ya kupiga kura katika kumchagua mrithi wa Ebrahim Raisi, ambaye alifariki baada ya kutokea ajali ya helikopta mwezi Mei.