1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMyanmar

Mtalaamu wa UN yaonya kuhusu "mauaji ya kimbari" Myanmar

4 Julai 2024

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa jimbo la Rakhine nchini Myanmar linakabiliwa na hali ya kuogofya sawa na ile ya kuelekea vurugu za mauaji ya halaiki miaka minane iliyopita dhidi ya jamii ya Warohingya

https://p.dw.com/p/4hsEM
Jimbo la Rakhine
Warohingya wamejipata kwenye kumbukumbuku ya matukio yaliosababisha mauaji ya kimbari mwaka 2016 na 2017Picha: STR/AFP

Thomas Andrews ameonya kuwa jimbo la Rakhine nchini Myanmar linakabiliwa na hali ya kuogofya sawa na ile ya kuelekea vurugu za mauaji ya halaiki miaka minane iliyopita dhidi ya jamii ya Warohingya walio wachache na wanaoteswa.

Soma pia: UN wachunguza kupotea kwa makaazi ya maelfu ya watu Myanmar

Akizungumza katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, Andrews, mjumbe maalumu wa Umoja huo kuhusu hali ya Myanmar, ametoa tahadhari kubwa kuhusiana na matukio ya hivi karibuni katika eneo la magharibi.

Andrews amesema jimbo la Rakhine ambapo utawala wa kijeshi nchini humo unalipoteza eneo hilo kwa kasi inatisha na kuongeza kwamba kwa Warohingya wanaokandamizwa na waliokwama kati ya pande zinazozozana, wamejipata kwenye kumbukumbuku ya matukio yaliosababisha mauaji ya kimbari mwaka 2016 na 2017.

Andrews, mtaalam huru aliyeteuliwa na baraza la haki za binadamu ambaye hazungumzi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, amesema jeshi nchini humo limekuwa likiwaandikisha maelfu ya vijana wa Rohingya na kuwahamasisha kupigana dhidi ya waasi wa Arakan.