1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya rais wa Haiti akamatwa

20 Oktoba 2023

Polisi nchini Haiti imemkamata afisa wa zamani na mshukiwa mkuu wa mauaji ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Jovenel Moise.

https://p.dw.com/p/4XmmB
Haiti I Foto des der verstorbenen haitianischen Präsidenten Jovenel Moise während seiner Gedenkfeier
Muombolezaji akiwa na picha ya aliyekuwa rais wa Haiti, Jovenel Moise, aliyeauwa mwezi Julai 2021.Picha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Msemaji wa *polisi ya Haiti, Garry Desrosiers, alisema siku ya Ijumaa (Oktoba 20) kuwa Joseph Badio alikamatwa katika kitongoji cha Petion Vile kilicho kwenye mji mkuu, Port-au-Prince.

Badio aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Sheria ya Haiti na pia katika kitengo cha serikali cha kupambana na rushwa na alifukuzwa kazi wiki kadhaa kabla ya mauaji, kwa madai ya ukiukwaji wa kanuni za maadili ambazo hazikubainishwa.

Soma zaidi: Seneta wa zamani wa Haiti akiri kupanga njama ya kumuuwa rais Jovenel Moise

Rais Moïse alipigwa risasi 12 alipokuwa nyumbani kwake mnamo Julai 7, 2021, mauaji yaliyoitumbukiza Haiti katika mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Watu kadhaa walikamatwa baada ya mauaji hayo, wakiwemo washukiwa 11 ambao kwa sasa wamezuiliwa nchini Marekani.