1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Raia wa Rwanda Nshimiye ashitakiwa kwa mauaji ya kimbari

27 Machi 2024

Raia wa Rwanda Eric Nshimiye anayeshutumiwa kwa kuwauwa watu kwa mapanga na kuwabaka wanawake wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, jana ameshtakiwa rasmi katika mahakama ya shirikisho ya Boston.

https://p.dw.com/p/4eAZ6
Vichwa na mifupa ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya Rwanda
Mafuvu ya vichwa vya binadamu yaliyohifadhiwa yakionyeshwa katika kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari huko Nyamata, ndani ya Kanisa Katoliki ambapo maelfu ya watu waliuawa wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda.Picha: SIMON MAINA/AFP

Kulingana na nyaraka za mahakama, Nshimiye ameshitakiwa kwa makosa yanayojumuisha habari za uwongo, kuzuia utekelezwaji wa haki na kudanganya chini ya kiapo.

Nshimiye alikuwa akiishi Ohio nchini Marekani.

Nshimiye, pia ameshitakiwa kwa kudanganya mara kwa mara kuhusu kuhusika kwake katika mauaji hayo ya kimbari hatua iliyomwezesha kuingia nchini Marekani kama mkimbizi mwaka 1995 na kisha kupata uraia wa nchi hiyo miaka minane baadaye.

Wakili wa umma huko Ohio, amesema hawezi kutoa tamko lolote kwasababu haishughulikii tena keshi hiyo na kwa ufahamu wake, ni kwamba wakili wa umma wa Boston bado hajakabidhiwa kesi hiyo.