1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

MSF yaimarisha uwepo wake nchini Haiti

6 Machi 2024

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF limetangaza leo kuwa linaongeza uwepo wake katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, kufuatia kuongezeka kwa vifo vinavyohusishwa na ghasia zinazozidi kuukumba mji huo.

https://p.dw.com/p/4dEeI
Vijana wakiinua mikono yao kuonyesha polisi hawajabeba silaha wakati wa operesheni dhidi ya magenge ya uhalifu Haiti
Vijana wakiinua mikono yao kuonyesha polisi hawajabeba silaha wakati wa operesheni dhidi ya magenge ya uhalifu HaitiPicha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

MSF imesema kuwa idadi ya majeruhi wanaohitaji matibabu kutoka kwa makundi ya misaada ya shirika hilo imeongezeka kwa kasi.

Mkuu wa ujumbe huo wa MSF Mumuza Muhindo Musubaho, amesema vitanda vyote 50 katika hospitali yao ya Tabarre vina wagonjwa tangu mwanzoni mwa mwezi Februari, lakini mnamo Februari 28 hali ilizidi kuwa mbaya na kulazimika kuongeza idadi ya vitanda hivyo kufikia 75.

Soma pia: Watu kadhaa wauawa Haiti baada ya Gereza Kuu kuvamiwa

Musubaho ameongeza kuwa kwasasa, wanapokea idadi ya wastani ya majeruhi 5 hadi 10 kwa siku na kwamba wamefikia mwisho wa uwezo wao.

Huku hayo yakijiri, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura baadaye leo kuhusiana na hali ya nchini Haiti.