1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya, Haiti zasaini makubaliano ya kutuma polisi

1 Machi 2024

Kenya na Haiti zimetia saini makubaliano ya kutuma polisi wa Kenya kuongoza ujumbe unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, kurejesha utulivu na usalama huko Haiti, taifa la Karibiani linalozongwa na machafuko ya magenge.

https://p.dw.com/p/4d5bU
Rais William Ruto wa Kenya
Rais William Ruto ametiliana saini na Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, makuballiano ya kupeleka askari 1,000 nchini Haiti.Picha: Dominika Zarzycka/NurPhoto/picture alliance

Rais William Ruto wa Kenya aliyasema hayo siku ya Ijumaa (Machi 1) baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, aliyewasili katika taifa hilo la Afrika Mashariki siku ya Alhamis.

Kulingana na Ruto, yeye na mgeni wake walijadiliana hatua zitakazofuata kuharakisha mchakato wa kupeleka polisi 1,000 wa Kenya nchini Haiti.

Soma zaidi: Maafisa wanne wa polisi wauawa Port-au-Prince

Lakini haikubainika wazi ikiwa makubaliano yaliyofikiwa yangelitimiza matakwa ya uamuzi wa mahakama uliotolewa mwezi Januari, ambao ulisema hatua ya kupeleka polisi wa Kenya kisiwani Haiti ni "kitendo kinachokinzana na sheria."

Kwenye nchini Haiti, polisi wanne waliuawa siku ya Ijumaa, huku mmoja wa viongozi maarufu wa magenge akitishia kumtimua madarakani Waziri Mkuu Henry.