1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa UK kuwapeleka wahamiaji Rwanda waenda mahakamani

5 Oktoba 2023

Serikali ya Uingereza itajaribu, wiki ijayo kuwashawishi majaji wa mahakama ya juu ya nchi hiyo kubadilisha hukumu yao kwamba mpango wa kuwahamishia wakimbizi nchini Rwanda ulikuwa kinyume cha sheria.

https://p.dw.com/p/4XAGN
Großbritannien Proteste gegen die Abschiebung nach Ruanda
Picha: Niklas Hallen/AFP/Getty Images

Mawakili wa serikali watahoji kwamba hukumu hiyo ilikuwa ya makosa. Kwa upande wao wanaowawakilisha wahamiaji kutoka Syria, Iraq, Iran na Sudan wanawataka majaji wabakie na msimamo uleule kwamba mpango huo wa kuwahamisha wahamiaji wa serikali ya Uingereza ulikuwa wa makosa.

Waziri mkuu Rishi Sunak na mawaziri wake  wanahoji kwamba mpango huo wa kuwahamishia wakimbizi nchini Rwanda uliozinduliwa mwaka uliopita na waziri mkuu wa hapo awali Boris Johnson utaivunja biashara ya wahalifu wanaosafirisha binadamu.