1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Monrovia: Umoja wa Mataifa umesema kampeni ya kuwavuwa silaha waasi...

27 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFxO
na wanamgambo wa serekali huko Liberia itaanza rasmi mapema zaidi. Uamuzi huo umechukuliwa huku kukiendelea kuweko mapigano ya hapa na pale katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi iliojionea vita viwili vya kienyeji. Afisa wa Umoja wa Mataifa alisema wanajeshi wa kuweka amani mwanzoni walitazamiwa kuanza kuwavuwa silaha waasi na wanamgambo wa serekali hapo Disemba 7. Karibu ya wapiganaji 800 wameshasalimu amri kwa maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, wakikabidhi bunduki zao pamoja na maroketi na risasi.