1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA: George Weah aongoza katika matokeo ya mwanzo ya uchaguzi

13 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESI

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi nchini Liberia yanaonyesha kwamba mcheza kandanda mashahuri barani Afrika, George Weah, amemshinda mpinzani wake wa karibu, waziri wa zamani wa fedha Ellen Johnson-Sirleaf.

Huku matokeo katika vituo 278 kati ya vituo 3,070 yakiwa yamejulikana, Weah anaongoza kwa aslimia 23.7 akifuatiwa na mwanauchumi, Ellen, aliye na asilimia 14.9. Kiongozi wa tume ya uchaguzi nchini humo, Frances Johnson Morris amesema ikiwa hali itaendelea namna hii, huenda kufanyike raundi ya pili ya uchaguzi.