MOGADISHU:Wababe wa kivita wasalimu amri na kuweka silaha chini
12 Julai 2006Matangazo
Wapiganaji 500 wa mfungamano wa wababe wa kivita ambao wamekuwa wanapambana na wanamgambo wa kiislamu wamejisalimisha na kukabidhi silaha zao.
Pande hizo mbili zimekuwa zinapigania udhibiti wa mji mkuu wa Somalia,Mogadishu. Watu wasiopungua 140 waliuawa katika mapigano hayo.
Walioshuhudia wanasema kuwa Umoja wa waislamu sasa unadhibiti asilimia 99 ya mji wa Mogadishu pamoja na miji mingine muhimu ya Somalia.