1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaRwanda

Mmoja afariki kwenye mkanyagano wakati wa kampeni Rwanda

24 Juni 2024

Mtu mmoja amekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mkasa wa mkanyagano uliotokea kwenye mkutano wa kampeni ya Rais wa Rwanda Paul Kagame.

https://p.dw.com/p/4hQn1
Rwanda | Kampeni | RPF | Paul Kagame
Maelfu ya wafuasi wa chama cha Rais Paul Kagame cha RPF wamekuwa wakihudhuria mikutano ya kampeni zake tangu ilipofunguliwa Jumamosi ya Juni 22, 2024. Picha: Jean Bizimana/REUTERS

Hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la taifa, kabla ya uchaguzi unaotarajiwa na wengi kuurefusha utawala wa miaka 24 wa kiongozi huyo.

Kampeni zilianza Jumamosi, huku Kagame akifanya mikutano katika maeneo ya Musanze na Rubavu, kaskazini ya Rwanda mwishoni mwa wiki. Shirika la habari la Rwanda lilisema watu 37 walijeruhiwa katika mkutano wa chama cha RPF.

Kagame amekuwa mtawala wa Rwanda tanfu kumalizika kwa mauaji ya kimbari ya 1994 ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 800,000, wengi wao Watsutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 66, ambaye aliingia madarakani 2000, atakabiliana na wapinzani wale wale alioshindana nao mwaka wa 2017.

Kiongozi wa chama cha Kidemokrasia cha Kijani Frank Habineza, na mwandishi habari wa zamani Philippe Mpayimana, anayeshiriki kama mgombea wa kujitegemea.