1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Rais wa zamani wa Urusi aionya NATO kuhusu vita vya nyuklia

19 Januari 2023

Rais wa zamani wa Urusi ambaye ni mwandani wa Rais wa sasa Vladimir Putin ameionya Jumuiya ya Kujihami ya NATO leo kwamba kuna hatari ya kuanza kwa vita vya nyuklia iwapo Urusi itashindwa katika vita nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4MQ5D
Russland | Innerer Kreis von Putin - Dmitry Medvedev
Picha: Yekaterina Shtukina/AP/picture alliance

Medvedev ambaye anahudumu kama naibu mwenyekiti katika baraza la usalama lenye nguvu la Rais Putin, ameyasema haya kupitia ujumbe aliouandika katika mtandao wa Telegram.

Kiongozi huyo wa zamani aliyehudumu kama rais wa Urusi kati ya mwaka 2008 hadi 2012, amesema jumuiya ya NATO  na viongozi wengine wa ulinzi ambao watakutana Ijumaa katika Kambi ya Kijeshi ya Ramstein nchini Ujerumani kujadili mikakati na uungwaji mkono wa juhudi za nchi za Magharibi kuishinda Urusi nchini Ukraine, wanastahili pia kufikiria kuhusiana na athari zitakazotokana na sera yao. Urusi na Marekani ndio wamiliki wakubwa wa zana za nyuklia, wakiwa na asilimia 90 ya zana za nyuklia duniani.