1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mkuu wa RSF nchini Sudan afanya ziara nchini Uganda

28 Desemba 2023

Mkuu wa kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan Jenarali Mohamed Hamdan Daglo, amesema Jumatano kuwa amekutana na rais wa Uganda Yoweri Museveni

https://p.dw.com/p/4adxd
Mkuu wa kikosi cha RSF - Jenerali Mohamed Hamdan Daglo wakati wa mkutano mjini Khartoum mnamo Juni 8, 2022
Mkuu wa kikosi cha RSF - Jenerali Mohamed Hamdan DagloPicha: Ashraf Shazly/AFP

Hii ni mara ya kwanza kwa Daglo kuthibitishwa kuonekana nje ya Sudan tangu vita kati ya kundi hilo la RSF na jeshi la Sudan kuzuka mwezi Aprili.

Daglo, ambaye habari zake tangu vita hivyo hazijulikani, amesema kupitia mtandao wa X kwamba wawili hao walizungumza kuhusu maendeleo nchini Sudan.

Soma pia:Mapigano mapya yazuka kusini mwa Sudan

Pia walizungumza kuhusu maono yake ya mazungumzo ya kumaliza vita.

Kupitia chapisho katika mtandao huo wa X, Museveni alithibitisha kufanyika kwa mkutano huo na kusema alimkaribisha Daglo nyumbani kwake Rwakitura.

Soma pia;RSF inatuhumiwa kufanya mauaji katika jimbo la Darfur

Jeshi la Sudan na RSF zimekuwa katika mzozo tangu katikati ya mwezi wa Aprili, ambao umesababisha uharibu mkubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Mapigano hayo yamesababisha wimbi la mauaji ya kikabila huko Darfur licha ya duru kadhaa za kidiplomasia za kuyasitisha.