1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mkuu wa jeshi la Sudan arudi nyumbani baada ya ziara Misri

30 Agosti 2023

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amerudi nyumbani baada ya kufanya ziara nchini Misri, ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuzuka kwa vita mwezi Aprili.

https://p.dw.com/p/4VjDl
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-BurhanPicha: Sudanese Army/AFP

Wakati mkuu huyo wa jeshi akisafiri Misri kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Abdel Fattah al-Sisi, madaktari na mashuhuda wameeleza kuwa watu 39 wameuawa, wengi wao wanawake na watoto katika shambulio la makombora eneo la Nyala, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini.

Eneo hilo linashuhudia makabiliano makali kati ya jeshi na vikosi vya msaada wa dharura RSF.

Akiwa Misri, al-Burhan alisema vikosi vyake vinapambana na "makundi ya waasi ambao wamefanya uhalifu wa kivita katika jaribio lao la kunyakua mamlaka."

Katika mkutano wao, ofisi ya Rais Abdel Fattah al-Sisi ilisisitiza msimamo thabiti wa Misri kusimama na Sudan na kuunga mkono usalama na uulivu wake.