1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 39 wauawa kwenye mapigano makali katika jimbo la Darfur

29 Agosti 2023

Watu wapatao 39 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa katika mapigano makali katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan.

https://p.dw.com/p/4VinY
Shirika la RSF limesema maelfu ya raia wamenaswa katika mji wa Njala kutokana na vurugu kati ya majeshi ya serikali na kikosi cha msaada wa dharura RSF.
Taarifa zimeeleza kuwa maelfu ya raia wamenaswa katika mji wa Njala kutokana na vurugu kati ya majeshi ya serikali na kikosi cha msaada wa dharura RSF.Picha: Ashraf Shazly/AFP

Kwa mujibu wa taarifa za upande wa upinzani nchini Sudan, wengi wa waathiriwa walikuwa wamejificha chini ya daraja katika mji wa Njala ambapo waliuawa katika shambulio la anga leo Jumanne.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulio hayo yaliyosababisha vifo vya raia.

Maelfu ya raia wamenaswa katika mji wa Njala kutokana na vurugu kati ya majeshi ya serikali na kikosi cha msaada wa dharura, RSF.

Rais na kiongozi wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amekataa kufanya mazungumzo na wanajeshi wapinzani. Mashirika ya misaada yamezahadharisha kwamba nchi ya Sudan inaelekea kwenye janga la kibinadamu.

Mamilioni ya watu wamelazimika kuikimbia nchi yao.