1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Mkutano wa uwekezaji Afrika wafanyika Berlin

20 Novemba 2023

Ujerumani ni mwenyeji wa kongamano la wawekezaji mjini Berlin chini ya mpango wa Ushirikiano wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda ya kundi la G20 na bara la Afrika. Mkutano huo unaongozwa na Kansela Olaf Scholz

https://p.dw.com/p/4ZAXv
Kanzler Scholz in Afrika | Kenia Geothermiewerk Olkaria
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amewaalika viongozi wa mataifa ya Kiafrika na yaliyostawi kiviwanda ya kundi la G20. Mpango huo ulianzishwa na Ujerumani wakati ikiwa mwenyekiti wa kundi hilo mwaka wa 2017 na unalenga kukuza uwezekaji zaidi wa kibinafsi katika mataifa ya Kafrika ili kuupiga jeki uchumi wao.

Soma pia: Ujerumani kufanya biashara ya nishati na Nigeria

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck pia anahudhuria mkutano huo wa kilele, pamoja na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, viongozi kumi wa mataufa ya Kiafrika na serikali, na zaidi ya mawaziri 30 kutoka barani humo.

Berlin Compact Africa mit Olaf Scholz
Nchi 13 za Kiafrika ni sehemu ya mradi huoPicha: JOHN MACDOUGALL/AFP

Heiko Schwiderowski, mkuu wa Chama cha Viwanda na Biashara cha Ujerumani anayehusika na masuala ya kanda ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, DIHK, anasema nia ya mpango huo wa ushirikiano na Afrika imeongezeka. Anasisitiza kuwa kongamano hilo la uwekezaji lenye wajumbe 800 linaelezewa kuwa kongamano kubwa kabisa la kibiashara kuwahi kufanyika kwenye ardhi ya Ujerumani.

Schwiderowski anasema viongozi wa kibiashara na kisiasa nchini Ujerumani wanatuma ishara muhimu, akiongeza kuwa kupanua mahusiano ya kiuchumi ni jitihada yenye manufaa.

Je, mpango huo umeleta mafanikio Afrika?

Mchambuzi kutoka Ghana Emmanuel Bendah anasema mipango kama hii ya ushirikiano wa G20 na Afrika ni nyenzo muhimu cha kutathmini uchumi wa Afrika na pia kutumika kama kifaa cha kupima maendeleo ya nchi za bara hilo, kwa sababu inawezesha kupata picha za nchi tofauti na kuona kinachoendelea nchini humo na kinachotatikana kuimarishwa.

Soma pia: Mkutano wa biashara baina ya Ujerumani na nchi za Afrika wakamilika mjini Johannesburg, Afrika Kusini

XN Iraki, profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Nairobi anayehusika na ukuaji uchumi, anasema bado ni mapema mno kufanya tathmini ya mradi huo. Anasema ni wazo zuri lakini miaka sita ni michache mno kujua athari zake. Profesa huyo anasema mazingira barani Afrika sio mazuri kwa uwekezaji wa kibinafsi.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Afrika Kusini ni mwenyekiti mwenza wa mkutano huoPicha: Tobias Schwarz/REUTERS

Iraki anasema Afrika haina miundo mbinu mizuri, kuna ukosefu wa utulivu wa kisiasa, na Imani kuwa nchi za Kiafrika zinahitaji kusaidiwa na mwingine. Hata hivyo anaamini kuwa ni muda mwafaka kwa nchi za Kiafrika kuchukua jukumu Zaidi.

Mtalaamu wa kiuchumi kutoka Ujerumani Robert Kappel ana mtizamo wa tahadhari. Ameiambia DW kuwa ipo haja ya kuufanyia mabadiliko muundo huo na kuangazia Zaidi ukweli kuwa maslahi ya Afrika yana jukumu kubwa. Maslahi ya Afrika yanajikita katika utanuzi wa viwanda na utengenezaji wa ajira.

Soma pia: Kansela Angela Merkel ahimiza uwekezaji barani Afrika

Kiasi ya mataifa 13 ya Kiafrika mpaka sasa yameungana katika mpango huo, Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia, Misri, Ethiopia, Ghana, Guinea, Morocco, Rwanda, Senegal, Togo na Tunisia. Kama mojawapo ya nchi kubwa kiuchumi barani Afrika, Afrika Kusini inashikilia uwenyekiti mwenza wa kongamano hilo.

Nchi nyingine kama vile Angola, Zambia, Nigeria na Kenya zinahudhuria kongamano hilo la Berlin kama wageni.

Makala hii ilitafsiriwa kutoka Kijerumani