1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaUingereza

Mkutano kuhusu teknolojia ya akili bandia kufanyika London

31 Oktoba 2023

Uingereza itaandaa mkutano wa kwanza wa kilele wa siku mbili utakaoanza kesho ili kuwaleta pamoja viongozi wa kisiasa, watafiti na wawakilishi wa sekta ya teknolojia ili kujadili maendeleo ya teknolojia ya akili bandia.

https://p.dw.com/p/4YDXR
Artificial intelligence, conceptual image Artificial intelligence. Conceptual illustration of a computer simulation and
Teknolojia ya akili bandia imepiga hatua kubwa katika miaka ya hivi karibuniPicha: Science Photo Library/IMAGO

Lengo la Uingereza ni kuwataka wadau wote kuwa na uelewa jumla juu ya kitisho cha teknolojia hiyo ikiwa ni pamoja na kupoteza nafasi za kazi, mashambulizi ya mtandaoni lakini pia uwezekano wa binaadamu kushindwa hapo baadaye kuidhibiti teknolojia hiyo ya akili bandia.

 Mkutano huo utafanyika huko Milton Keynes mjini London.

Soma pia: Ulimwengu wa teknonolojia unakuwa kwa kasi na matumizi ya Akili ya kubuni nayo yanazidi kuongezeka kila uchwao

Kabla ya mkutano huo, mataifa saba yenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani G7, yalikubaliana siku ya Jumatatu nchini Japan kuhusu kuwepo kwa "kanuni" zinazokusudiwa makampuni yanayotengeneza mifumo ya hali ya juu zaidi ya teknojia ya akili bandia (AI).