1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Guterres aunda jopo kuangazia matumizi ya Akili ya kubuni

27 Oktoba 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameunda jopo la wataalamu watakaoandaa mapendekezo juu ya udhibiti wa kutumia Akili ya kubuni ama Artificial Intelligence.

https://p.dw.com/p/4Y5Dj
Teknolojia ya Akili ya kubuni imekuwa ikishika kasi na hasa katika mataifa yaliyoendelea na kuibua kitisho licha ya manufaa yake.
Teknolojia ya Akili ya kubuni imekuwa ikishika kasi na hasa katika mataifa yaliyoendelea na kuibua kitisho licha ya manufaa yake.Picha: Bastian/Caro/picture alliance

Guterres amesema licha ya teknolojia hii ya Akili ya kubuni kuwa muhimu lakini inatishia demokrasia na haki za binaadamu.

Guterres amelitaka jopo hilo kuharakisha mchakato wa kuandaa mapendekezo yatakayoainisha namna ya kudhibiti matumizi ya AI hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2023, kuanzia kitisho hadi fursa zinazokuja na teknolojia hiyo.

Guterres amechagua jopo la wataalamu 40 wa teknolojia na ulinzi wa taarifa binafsi, wakati akiashiria mashaka yanayoibuliwa na teknolojia hiyo ambayo ni pamoja na upotoshwaji wa taarifa, ubaguzi, ufuatiliaji na uingiliaji wa faragha.​