1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKenya

Mkataba wa kiuchumi kati ya Kenya na Ulaya kuanza karibuni

31 Mei 2024

Mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Kenya na Umoja wa Ulaya (EPA) unatazamiwa kuanza kufanya kazi wakati wowote kutokea sasa.

https://p.dw.com/p/4gVRU
Droni ikimwaga mbolea kwenye shamba la chai nchini Kenya
Droni ikimwaga mbolea kwenye shamba la chai nchini lililopo Kipkebe nchini Kenya. Chai ni miongoni mwa mazao yanayouzwa na Kenya barani Ulaya.Picha: PATRICK MEINHARDT/AFP/Getty Images

Hatua hiyo itaanza kutekelzwa baada ya baraza la jumuiya hiyo kupitisha na kuhitimisha mchakato wa maridhiano.

Mkataba huo utaiwezesha Kenya kuuza bidhaa zozote isipokuwa silaha kwenye soko la Ulaya bila vikwazo na bila kulipishwa kodi. Kwa upande mwengine, Ulaya nayo itapata soko jipya nchini Kenya litakalofunguliwa kwa awamu.

Umoja wa Ulaya na Kenya zilitiliana saini mkataba huo wa ushirikiano Desemba mwaka uliopita.

Mwaka 2021, Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya uenyekiti wa Kenya, iliridhia kwamba kila nchi mwanachama itekeleze kivyake mkataba huo wa ushirikiano wa uchumi na Umoja wa Ulaya.