1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hezbollah yaendeleza mashambulizi ya kisasi dhidi ya Israel

15 Juni 2024

Kundi la Hezbollah la Lebanon limeendeleza mashambulizi ya kisasi dhidi ya ngome za jeshi kaskazini mwa Israel, huku mtu mmoja akiuawa nchini Lebanon.

https://p.dw.com/p/4h5Jo
Videostill | Hezbollah threat in northern Israel
Israel na Hezbollah, mshirika wa kundi la Kipalestina la Hamas, zimeshambuliana karibu kila siku tangu vita vya GazaPicha: Rebecca Ritters/DW

Hezbollah imesema kuwa imeishambulia kambi ya kijeshi ya Meron kaskazini mwa Israel kwa kutumia makombora ya kuongozwa, na kurusha droni za mashambulizi kuelekea kambi nyingine ya jeshi la Israel, kama sehemu ya majibu ya shambulizi na mauaji yaliofanywa na adui kijijini Jouaiyya.

Soma pia: Kundi la Hezbollah ladai kuishambulia Israel kwa roketi

Israel na Hezbollah, ambalo ni mshirika wa kundi la Kipalestina la Hamas, zimeshambuliana karibu kila siku tangu shambulio la Hamas la Oktoba 7 nchini Israel, lililosababisha vita vya Gaza.

Kamanda wa juu wa Hezbollah Taleb Abdallah aliuwa na Israel katika kijiji cha Jouaiyya siku ya Jumanne.