1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yaandaa mkutano kuyakutanisha makundi ya kisiasa Sudan

29 Mei 2024

Misri itaandaa mkutano utakaoyaleta pamoja makundi ya kisiasa ya kiraia ya Sudan mnamo mwezi Ujao wa Juni pamoja na wajumbe wa kikanda na kimataifa.

https://p.dw.com/p/4gPq0
Jenerali  Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan na Mohamed Hamdan Dagalo
Kiongozi wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan  na kiongozi wa kundi la wanamgambo la RSF Mohammed Hamdan Dagalo.Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Hayo yameelezwa jana na wizara ya mambo ya kigeni ya nchi hiyo. Mkutano huo unalenga kutafuta makubaliano kati ya makundi ya kiraia ya Sudan  kuhusu njia za kujenga amani thabiti na ya kudumu.

Watu 85 wauwawa kufuatia mapigano makali Sudan

Mpaka sasa mataifa ya kikanda na kimataifa ikiwemo Marekani, Misri na Saudi Arabia yamejaribu kutafuta makubaliano ya amani kati ya pande zinazopigana,bila ya mafanikio.

Tangu mwaka 2023 Sudan iko kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la serikali likiongozwa na jenerali Abdel Fattah al-Burhan  na kundi la wanamgambo la RSF linaloongozwa na Hamdan Dagalo.Maelfu ya raia wanakadiriwa kuuwawa.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW