1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri kuongoza mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza

7 Julai 2024

Misri imesema itakuwa mwenyeji wa ujumbe wa Israel na Marekani utakaokutana nchini humo kwa mazungumzo ya vipengele muhimu katika mpango wa kusitisha mapigano kati ya Israel na Palestina

https://p.dw.com/p/4hz9p
Rais wa Misri  Abdel-Fattah al-Sisi
Misri itakuwa mwenyeji wa mazungumzo ya kujaribu kusitisha mapigano Gaza Picha: THIBAULT CAMUS/AFP via Getty Images

Mazungumzo hayo yatajumuisha makubaliano ya kuwaachia mateka, hii ikiwa ni kulingana na televisheni ya taifa nchini Misri. 

Juhudi za kufikia makubaliano hayo zilianzishwa baada ya kukwama kwa wiki kadhaa. Taarifa zaidi zinasema kwamba Misri pia inafanya majadiliano na wanamgambo wa Hamas kama sehemu ya mikakati ya kufanikisha makubaliano ya kusitisha mapigano. 

Israel inaendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza

Mazungumzo hayo ambayo sio ya moja kwa moja yanayosimamiwa na Marekani Misri na Qatar yalikwama kwa wiki kadhaa huku Hamas ikisisitiza kwamba Israel inapaswa kwanza kusitisha vita vyake Gaza ili iwaachie mateka 120 inaowashikilia.