1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miito ya kulipiza mauaji ya Haniyeh yatolewa katika mazishi

1 Agosti 2024

Iran imefanya mazishi ya kiongozi mkuu wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh huku ikiahidi kulipiza kisasi. Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khemenei aliongoza ibada ya mazishi ya Haniyeh kabla ya kuzikwa huko Qatar.

https://p.dw.com/p/4izYr
Maziko ya Ismail Haniyeh
Iran imefanya mazishi ya kiongozi mkuu wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh huko QatarPicha: Iranian Leader Press Office/Anadolu/picture alliance

Kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khemenei aliongoza ibada ya mazishi ya Haniyehkabla ya kuzikwa huko Qatar, na tayari amenukiliwa awali akitishia kulipiza vikali mauaji ya kiongozi huyo aliyeuawa kwenye shambulizi, la huko Tehran.

Mwandishi wa AFP ameripoti kuwa maelfu wa waombolezaji walifurika katika eneo la chuo kikuu mjini Tehran, wakiwa na mabango yenye picha ya Haniyeh na bendera za Palestina.

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian na mkuu wa Kikosi cha Mapinduzi, Jenerali Hossein Salami pia walihudhuria.

Soma pia: Je Kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh ni nani?

Mkuu wa mambo ya kigeni wa Hamas Khalil al-Hayya, aliapa kwenye shughuli hiyo kuendeleza kauli mbiu ya Haniyeh ya kutoitambua Israel na wataendelea kupambana nayo hadi itakapoondoka kwenye ardhi ya Palestina.