1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MICHEZO YA 28 YA OLIMPIK YAMALIZIKA:AFRIKA YANYAKUA MEDALI 35 TU SAWA NA SYDNEY 2000.

Ramadhan Ali30 Agosti 2004
https://p.dw.com/p/CHZt

MICHEZO YA OLIMPIK YA ATHENS YAFUNGA PAZIA:

Baada ya mbio za kusisimua na kutatanisha za marathon ambamo ushindi haukwenda kwa bingwa wa rekodi ya dunia mkenya paul tergat alietoka mikono mitupu bila ya medali, pazia la michezo ya 28 ya Olimpik mjini Athens, iliorudi nchini ya asili-ugiriki, lilifungwa na mwenge ukazimwa na kuwaita wavulana na wasichana kujumuika tena kwa michezo ya 29 ya olimpik miaka 4 kutoka sasa mjini Beijing, china.

Mamia ya wanariadha wake kwa waume kutoka nchi 202 mbali mbali duniani,chini ya mshindo wa ngoma na nyimbo za kigiriki walichanganyika katika kitovu cha Uwanja mkuu wa olimpik huko Athens jana usiku wakipepea bendera za mataifa yao na medali zao shingoni,dhahab ,fedha na shaba.

Mwishoe , michezo hii iliojionea ulinzi mkalöi kabisa, kutoka baharini,nchi kavu na angani,ilizima mwenge wa olimpik uliowaka uwanjani kwa muda wa siku 17 na mabaki ya mwenge huo kukabidhiwa jiji la Beijing,utakaoandaa michezo ijayo ya 29 mwaka 2008. Beijing iliwatumbuiza watazamaji kwa ngoma ya kienyeji kuwatayarisha na makaribisho yao yatakavyokua 2008.

BARA LA AFRIKA NA MICHEZO YA ATHENS:

wakati Afrika iliendelea kutamba katika medani ya riadha na hasa kuanzia masafa ya kati hadi marefu na kuibua mabingwa wasio tazamiwa na kujipatia medali kama Zimbabwe na afrika Kusini kutoka hodhi la kuogolea, Afrika haikupiga hatua kubwa ukilinganisha na nguvu zake zilivyokua miaka 4 nyuma katika michezo ya Sydney,Austzralia:

Wanariadha wa afrika wanarudi nyumbani kutoka Athens wakiwa na medali 9 za dhahabu,11 za fedha na 13 za shaba.Jumla ya medali 35.japan pekee imenyakua medali 37-2 kupita hizo za Afrika. Miaka 4 nyuma huko Sydney, Australia,Afrika ilikusanya pia medali 35-9 za dhahabu,11 za fedha na 15 za shaba.

Licha lakini ya orodha ndogo ya medali ukilinganisha na mataifa mengine makuu,Afrika ilisisimua mno katika medani ya riadha:Muethiopia Kennenisa Bekele,amepiga mhuri wake huko Athens kuwa ndie mfalme mpya wa mbio za riadha anaefuata nyayo za Haile Gebre-selassie ambae sasa atahamia mbio za marathon.Bekele hakutimiza matarajio ya mzee Miruz Yifter ya kushinda medali za dhahabu katika masafa yote 2: mita 5000 na 10,000 hatahivyo,ndie jogoo jipya linalowika kutoka Ethiopia na Afrika.Wasichana wa Ethiopia akina Dibaba waliwika katika mita 5000,alkini sio katika mita 10.000 au marathon.

Hicham El Gerrouj wa Morocco mmoja kati ya mabingwa wakubwa katika masafa ya mita 1500 na bingwa wa rekodi ya dunia,mwishoe ametamba pia katika medani ya Olimpik, baada ya majaribio 2 ya kutoka mikono mitupu.Ameshinda kwanza mita 1500 na baadae mita 5000 na hii ikiwa ni historia kuchanganya mataji yote 2.

Kuna wasichana 2 wengine wa afrika waliosangaza michezo hii:Muogoleaji kutoka zimbabwe Kirsty Coventry,ameibuka mshindi wa medali ya dhahabu kutoka hodhi la kuogolea.Rais Robert Mugabe maarufu kwa kupambana vikali na wazungu wachache nchini Zimbabwe,zamani Rhodesia, alimkaribisha msichana huyu wa kizungu nyumbani kwa makaribisho maalumu na kitita cha dala 50,000 na pasi ya kibalozi.

Msichana wa cameroun Francois Mbango Etone, alitamba katika kuruka mara 3 –triple jump.Alimshinda bingwa alietazamiwa kuwika Tatyana Lebedeva aliemaliza 3.

Afrika ilitazamiwa kuwika katika mbio za marathon, kwani sio tu bingwa wa rekodi ya dunia anatoka Afrika-mkenya Paul Tergat, bali pia kwa kuwa Kenya,licha ya kutamba katika masafa marefu katika olimpik haikuwahi kutwaa medali ya dhahabu katika mbio za marathon.

Ila kali zimetolewa nyumbani Kenya juu ya kurudi na medali 1 tu ya dhahabu kwa Kenya kutoka michezo ya Athens .Kenya imeibuka nafasi ya 3 katika Afrika nyuma ya Ethiopia na Morocco. Ethiopia imenyakua medali 7-2 dhahabu,3 fedha na 2 shaba.Kenya 1 dhahabu, 4 fedha na 3 shaba.

China imeibuka dola la pili kuu limetwaa jumla ya medali 35 za dhahabu,39 za fedha na 29 za shaba-zote 103, wanariadha 407 kutoka china, ile ya miaka 4 nyuma huko Sydney,Australia ya medali 59 kati ya hizo 28 za dhahabu.China leo imelipiku dola kuu la zamani la lakini ni 27 tu za dhahabu.