1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiSenegal

Waziri wa sheria Senegal: Kifungo cha Sonko hakitobadilishwa

30 Agosti 2023

Waziri wa sheria wa Senegal Ismaila Madior Fall amesema uamuzi wa kufungwa kwa kiongozi wa upinzani nchini humo Ousmane Sonko kutokana na sakata la ufisadi lililokuwa linamkabili ni wa mwisho.

https://p.dw.com/p/4Vm2Q
Senegal Ousmane Sonko Oppositionsführer
Picha: Cooper Inveen/REUTERS

Katika mahojiano yaliyochapishwa mtandaoni leo na jarida la Jeune Afrique, Fall amesema iwapo Sonko angetaka hukumu dhidi yake ifutiliwe mbali basi angefika mahakamani mwenyewe ila kwa kuwa hakufanya hivyo basi hukumu iliyotolewa ndiyo ya mwisho.

Sonko alipatikana na hatia ya ubakaji mnamo Juni mosi hukumu iliyopelekea machafuko nchini humo yaliyosababisha vifo vya watu 16.

Soma zaidi:Senegal: Sonko alazwa chumba cha wagonjwa mahututi

Mnamo Julai alikamatwa kwa madai mengine ila wakati wa kusomewa hukumu yake, alizuiwakutoka nyumbani kwake na maafisa wa usalama ila hakupewa kifungo.

Mamlaka zimekivunjilia mbali chama chake na kuwakamata mamia ya wanachama na wafuasi wake.