1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEcuador

Watu watano wameuawa Ecuador

5 Juni 2023

Watu watano wameuawa na wengine wanane wamejeruhiwa katika mji wa Guayaquil nchini Ecuador.

https://p.dw.com/p/4SCCQ
Ecuador Mord in Guayaquil
Picha: Santiago Arcos/REUTERS

Uhalifu huo umefanywa na makundi ya watu wenye silaha wanaohusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya. Kanali wa Polisi eneo hilo Fabary Montalvo amesema miongoni mwa waliouawa ni askari polisi aliyepigwa risasi kichwani.

soma pia': Watu 15 wamekufa kutokana na tetemeko la ardhi huko Ecuador na Peru

Mji wa bandari wa Guayaquil unapatikana kwenye pwani ya kusini mwa Ecuador.

Magenge hasimu ya ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya Kokeini yamekuwa yakigombea udhibiti wa mji huo wa kimkakati na kusababisha umwagaji mkubwa wa damu. Mwaka jana mamlaka ya Ecuador ilikamata tani 200 za dawa za kulevya.