1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles III ziarani Kenya

31 Oktoba 2023

Mfalme Charles III wa Uingereza na mkewe Malkia Camilla wameanza leo ziara yao ya kiserikali ya siku nne nchini Kenya.

https://p.dw.com/p/4YE8Y
Königlicher Besuch in Kenia – Tag eins
Rais William Ruto wa Kenya akimkaribisha Mfalme Charles III tarehe 31 Oktoba 2023.Picha: Arthur Edwards/The Sun/empics/picture alliance

Mfalme Charles III anakabiliwa na miito ya kumtaka aombe radhi kuhusiana na historia ya umwagaji damu uliosababishwa na ukoloni wa Uingereza.

Ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo wa nchi mwenye umri wa miaka 74 katika taifa la Kiafrika na Jumuiya ya Madola tangu alipovishwa taji la Ufalme Septemba mwaka jana baada ya kifo cha mama yake, Malkia Elizabeth II.

Soma zaidi: Mfalme Charles III alihutubia Bunge la Ufaransa

Mfalme Charles III na mkewe, ambao waliwasili Kenya jana usiku, walikaribishwa katika hafla rasmi leo asubuhi na Rais William Ruto wa Kenya katika Ikulu ya Nairobi.

Soma zaidi: Tume ya haki Kenya yamtaka Mfalme Charles aombe msamaha

Ruto ameisifu ziara hiyo akisema ni fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Ubalozi wa Uingereza umesema ziara hiyo, inayofuatia safari za Ujerumani na Ufaransa mapema mwaka huu, itaangazia ushirikiano thabiti uliopo kati ya Uingereza na Kenya.

Lakini pia itatambua mambo machungu zaidi ya uhusiano wa kihistoria kati ya Uingereza na Kenya.

Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inajiandaa kuadhimisha miaka 60 ya uhuru Desemba mwaka huu.