1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles III alihutubia Bunge la Ufaransa

21 Septemba 2023

Mfalme Charles III wa Uingereza aliye ziarani Ufaransa amelihutubia Bunge la nchi hiyo na kusema Ufaransa na Uingereza zina jukumu la pamoja katika migogoro kama vita vya Ukraine na mabadiliko ya tabianchi

https://p.dw.com/p/4Wf8y
Frankreich | Besuch von King Charles III
Picha: Emmanuel Dunand/Pool/AP/picture alliance

Ametoa wito pia wa kuimarisha mahusiano kati ya mataifa hayo.Mfalme Charles na mkewe Camilla walipokelewa katika siku ya kwanza ya ziara yao kwa sherehe katika "Arc de Triomphe" na kukaribishwa chakula cha jioni na mwenyeji wao, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ikulu ya Versailles. 

Mfalme Charles III kuimarisha uhusiano na Ufaransa

Mfalme huyo atavitembelea vitongoji vya kaskazini mwa mji mkuu Paris na atalizuru Kanisa kuu la Notre-Dame lililoharibiwa kwa moto. 

Rais Macron amemuhakikishia Mfalme Charles kuwa licha ya Uingereza kujiondowa ndani ya Umoja wa Ulaya, bado itaendelea kuwa sehemu ya kanda hiyo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za pamoja.