1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel atetea ziara ya Dalai Lama

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQG7

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amejitetea dhidi ya shutuma zinazoendelea juu ya ziara ya Dalai Lama hapo mwezi wa Septemba.

Merkel ameliambia gazeti la Bild kwamba anaamuwa nani wa kukutana naye na wapi.Serikali ya China ilikasirishwa na ziara hiyo na tokea wakati huo imefuta mikutano kadhaa ya ngazi ya juu.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema kwamba serikali inafanya kila iwezalo kutuliza usumbufu uliosababishwa na ziara hiyo.