1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu kuwania tiketi ya kufuzu robo fainali

3 Agosti 2020

Mechi za ligi ya mabingwa Champions League pamoja na mechi za ligi ya Ulaya Europa League zinatifua vumbi tena wiki hii huku timu zikiwania tiketi ya kufuzu kwa robo fainali ya michuano hiyo.

https://p.dw.com/p/3gMHr
Großbritannien Fußball | Manchester City | Etihad Stadium
Picha: picture-alliance/dpa/Actionplus

Mnamo siku ya Ijumaa, itakuwa ni zamu ya mabingwa wa Seria A Juventus kuchuana na Olympic Lyon ya Ufaransa huku nayo Manchester City ya England ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya mabingwa wa Uhispania Real Madrid alafu siku ya Jumamosi Barcelona itapambana na Napoli nayo Bayern Munich itaialika Chelsea katika uwanja wa Allianz Arena.

Hata hivyo, kuna hali ya ati ati iwapo Barcelona itaruhusiwa kuutimia uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp kutokana na hofu ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona jimboni Catalonia.

Washindi wa mechi hizo watajiunga na Paris Saint Germain, Atletico Madrid, RB Leipzig na Atalanta ambazo tayari zimefuzu katika hatua ya robo fainali.