Mazungumzo ya ZANU na upinzani yakwama Zimbabwe
17 Desemba 2007Matangazo
HARARE
Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe kimesema hapo jana mazungumzo na serikali ya Rais Robert Mugabe juu ya katiba mpya yamekwama.
Chama tawala cha ZANU-PF na makundi mawili ya chama kikuu cha upinzani cjha MDC yamekuwa na mazumgumzo chini ya usuluhishi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC ambayo imempa jukumu Rais Mbeki wa Afrika Kusini kujaribu kumaliza mzozo wa kiuchumi na kisiasa ulioikumba nchi hiyo.
ZANU-PF na upinzani vimekubaliana juu ya haja ya kuwa na katiba mpya,marekebisho ya sheria kali za usalama na vyombo vya habari na kukomesha kwa matumizi ya nguvu ya kisiasa ili kuhakisha kwamba uchaguzi unaotazamiwa hapo mwaka 2008 unakuwa huru na wa haki.