1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya amani ya Burundi kuanza jumapili ijayo daresalam

12 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFEB

Mazungumzo kati ya serikali ya Burundi na kundi pekee la wanamgamb o nchini Burundi FNL,yanatazamiwa kufanyika Daresalaam Tanzania jumapili ijayo.Duru za kuaminika toka pande zote mbili zimesema hii leo.Msemaji war ais Domitien Ndayizeye wa Burundi Pancrace Cimpaye amesema wamealikwa kuhudhuria mazungumzo hayo.Rais Domitien Ndayizeye anatazamiwa kushiriki katika kikao cha ufunguzi kitakachohudhuriwa pia na mkuu wa FNL Agathon Rwasa.

Burundi inafanya juhudi za kumaliza vita vya miaka 12 vya wenyewe kwa wenyewe vilivyogharimu maisha ya zaidi ya watu laki tatu.Tangu zaidi ya mwaka mmoja uliopita,FNL limekua kundi pekee kati ya sabaa ya waasi wa zamani,linaloendeleza mapambano kwa mtutu wa Bunduki.