1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya kuiwekea viongozi Niger

31 Agosti 2023

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wamezungumzia wasiwasi mkubwa walionao kuhusu mapinduzi ya kijeshi yanayoongezeka barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4Vos4
Spanien Toledo | Treffen der EU Außenminister
Picha: Andrea Comas/AP/picture alliance

Katika mkutano unaojadili juu ya vikwazo vinavyowalenga watawala wa kijeshi nchini Niger waliotwaa madaraka kwa nguvu  mwezi mmoja uliopita. 

Wengi wa mawaziri hao wamesema kwamba bara la Afrika linapaswa kushughulikia  changamoto zake.

Waziri wa mambo ya nje wa Italia, Antonio Tajani amesema Umoja wa Ulaya unapaswa kutetea demokrasia kwa njia za kidiplomasia  na sio kupitia matumizi ya silaha. 

Soma pia:Umoja wa Ulaya kuijadili Niger katika mkutano maalum

Tajani ametahadharisha dhidi ya uingiliaji wa kijeshi nchini Niger akisema kwamba ni hatua itakayosababisha hatari ya kuwaacha watu wengi zaidi bila makaazi katika eneo la Sahel.

Mawaziri hao wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana Toledo Uhispania wamesema ni muhimu kuiunga mkono jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.

Mawaziri hao pia wanajadili pamoja na waziri mwenzao wa Ukraine, kuhusu kampeini ya juhudi za  kidiplomasia ya Ukraine kumaliza uvamizi wa  Urusi nchini humo.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW