1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaziri wa EU washindwa kufikia makubaliano kuhusu Ukraine

29 Mei 2024

Mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels walishindwa kufikia makubaliano kuhusu kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za mataifa hayo kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4gPjD
Umoja wa Ulaya
Bendera za Umoja wa Ulaya na Ukraine zikipepea nje ya makao makuu ya Umoja huo mjini Brussels Picha: Lukasz Kobus/European Union | CC BY 4.0

Nchi hizo zilishapitisha makubaliano ya pamoja ya kuipatia msaada wa silaha nchi hiyo.

Hata hivyo baadhi ya nchi wanachama zimetoa silaha zao kwa masharti ya kuitaka Ukraine isizitumie kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi.

Ulaya yagawanyika kuhusu Ukraine kutumia silaha za magharibi ndani ya Urusi

Serikali ya mjini Kiev inasisitiza kwamba wanajeshi wake wanahitaji kuruhusiwa kushambulia ndani ya Urusi kwa sababu vikosi vya nchi hiyo vinashambulia kutoka ndani ya ardhi yake kwenye maeneo ya mipaka.

Rais Emmanuel Macron ambaye jana alikutana na Kansela Olaf Scholz karibu na mji wa Berlin aliunga mkono hatua ya kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za nchi za Magharibi kushambulia ngome za kijeshi za Urusi ndani ya nchi hiyo,wakati Scholz akijizuia kutowa msimamo kama huo,japo alisema Ukraine inayo haki ya kijilinda.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW